• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Serena kupimana nguvu na Simona Halep kwenye fainali za Wimbledon

    (GMT+08:00) 2019-07-12 10:08:51

    Simona Halep ndio kikwazo cha mwisho kabisa kilichobaki mbele ya Serena Williams cha kuweza kufikia ndoto zake za kuweka rikodi ya kuchukua taji la Grand Slam kwenye uwanja wa Margaret baada ya wote wawili kuweka rikodi safi ya ushindi kwenye nusu fainali ya Wimbledon hapo jana. Williams ambaye ni bingwa mara saba alimwangusha kiubwete MCzech Barbora Strycova, ambaye hii ni kampeni yake ya kwanza kabisa kwenye nusu fainali za Grand Slams kwa mchezaji mmoja mmoja iliyodumu chini ya saa moja kwa kushindwa kwa alama 6-1, 6-2. Halep ambaye ni mchezaji namba moja wa zamani alimenyana na M-Ukrainia Elina Svitolina mechi iliyoendelea kwa muda mrefu kidogo, na kuondoka na ushindi wa 6-1, 6-3 na kuwa Mromania wa kwanza mwanamke kufika fainali za Wimbledon.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako