• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda na Tanzania kuzindua kongamano la biashara

  (GMT+08:00) 2019-07-12 19:09:38
  Serikali ya Uganda imesema wamezindua kongamano la biashara kati ya Uganda na Tanzania. Waziri wa masuala ya kikanda wa Uganda Daktari Phillomena Mateka amesema lengo la kongamano hilo ni kuunda jukwaa la kibiashara kwa mashirika ya biashara kutoka nchi zote mbili. Kauli mbiu ya kongamano hilo ambalo linatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 4-6 katika jumba la Mwalimu Julius Nyerere ni "kupiga jeki ukuaji wa biashara na uwekezaji na maendeleo endelevu. Kongamano hilo litawaleta pamoja wafanya biashara, watunga sera na wadau wengine kukumbatia nafasi zilizopo katika nchi zote mbili. Balozi wa Uganda nchini Tanzania Richard Kabonero amesema kwenye kongamano hilo washiriki watapata fursa ya kutangamana na rais wa Uganda Yoweri Museveni na mwenzakje wa Tanzania John Pombe Magufuli. Nchi zote mbili zinalenga kuondoa vikwazo vya kibiashara ili kuwawezesha wafanya biashara kukumbatia nafasi zilizopo katika nchi hizo mbili.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako