• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuyawekea vikwazo makampuni ya Marekani yanayohusika na kuiuzia silaha Taiwan

  (GMT+08:00) 2019-07-12 20:21:21

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema China itayawekea vikwazo makampuni ya Marekani yanayoshiriki kuiuzia silaha Taiwan.

  Bw. Geng amesema hayo baada ya Marekani kutangaza mpango wa kuiuzia Taiwan silaha zenye thamani ya dola bilioni 2.2 za kimarekani. Bw. Geng amesema kitendo cha Marekani ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa, kanuni za kawaida za uhusiano wa kimataifa, mamlaka ya China, kanuni ya China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani. Bw. Geng amesema China itachukua hatua hiyo ili kulinda maslahi ya taifa.

  Bw. Geng pia amesema jaribio lolote la kuiyumbisha Hong Kong halitafanikiwa, na kuwa China inapiga vikali uingiliaji wa Marekani wa mambo ya Hong Kong na mambo ya ndani ya China. Bw. Geng amesema hayo akitoa maoni kuhusu mshauri wa mambo ya usalama wa Marekani Bw. John Bolton, makamu wa rais wa Marekani Bw. Mike Pence na Waziri wa mambo ya nje Bw Mike Pompeo, kukutana na mfanyabiashara wa Hong Kong Bw Jimmy Lai kujadili marekebisho ya sheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako