• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatenga hekta elfu 2 kwa ajili ya uwekezaji kwenye viwanda vya korosho

    (GMT+08:00) 2019-07-13 17:19:04

    Mamlaka nchini Tanzania zimetenga hekta 2000 za ardhi kwa ajili ya wawekezaji wenye lengo la kuwekeza kwenye mashamba ya korosho na viwanda vya kuchakata zao hilo, ili kuliongezea thamani.

    Akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) mkoani Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Georfrey Zambi amesema kuna fursa nyingi za uwekezaji kwenye mashamba na viwanda vya kuchakata zao hilo.

    Bwana Zambi amesema juhudi zinazofanyika mkoani Lindi zimeongeza uzalishaji wa korosho, na kushuhudia miche mipya milioni 7 ikipandwa. Naibu waziri wa kilimo wa Tanzania Bw. Omary Mgumba amesema serikali ilikuwa na lengo la kuongeza uzalishaji wa korosho na kufikia tani milioni moja kwa mwaka wa fedha 2023 - 2024, lilikuwa ni ongezeko la tani laki 3.13 ikilinganishwa na uzalishaji wa msimu wa 2017 – 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako