• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Uingereza zasisitiza nia ya kulinda mazingira na kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2019-07-13 17:19:33

    Uingereza na Kenya zitawekeza kwenye programu za pamoja zenye lengo la kutafuta njia ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kulinda mazingira.

    Waziri wa maendeleo ya kimataifa wa Uingereza Bw. Rory Stewart ambaye yuko kwenye ziara ya siku mbili nchini Kenya, amesema kupambana na ongezeko la joto ni sehemu muhimu ya mahusiano ya pande mbili kati ya Uingereza na nchi nyingine. Ameipongeza Kenya kwa kuwa kwenye nafasi ya uongozi katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa, na kuwataka wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali katika juhudi hizo.

    Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bibi Monica Juma amesema Kenya itaendelea kuimarisha uhusiano wa kunufaishana na Uingereza, na kuimarisha uhusiano huo ili kuhimiza uwekezaji kwa ajili ya manufaa ya watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako