• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alaani shambulizi la kigaidi nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2019-07-13 17:31:00

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani shambulizi la kigaidi lililotokea jana katika hoteli moja kusini mwa Somalia, ambalo limesababisha vifo vya watu wasiopungua 10.

    Bw. Guterres ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya wahanga wa shambulizi hilo. Pia amesisitiza tena kuwa Umoja wa Mataifa unawaunga mkono wananchi wa Somalia katika kutafuta mustakabali wenye amani.

    Mapema ya jana, wapiganaji wenye silaha walishambulia hoteli moja kwenye mji wa bandari wa Kismayu, kwa gari lililokuwa limejaa mabomu kugonga lango la hoteli. Hoteli hiyo hutembelewa zaidi na mawaziri na wabunge. Habari zinasema baadhi ya wabunge walikuwa wanakaa kwenye hoteli hiyo wakati wa shambulizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako