• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanne washukiwa kuwa majambazi wauawa na polisi Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-07-13 18:17:47

    Kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani nchini Tanzania Bw. Wankyo Nyigesa amesema polisi wameua watuhumiwa wanne wa ujambazi katika tukio kali la ufyatuaji wa risasi lililotokea Alhamisi.

    Bw. Nyigesa amesema hayo kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya polisi wa mkoa wa Pwani, akiongeza kuwa polisi waliwazingira watuhumiwa hao wakati walipojaribu kuvamia na kuiba kutoka mkadarasi wa mradi wa kujenga bandari kavu katika Kwala, eneo la Mlandizi mkoani humo, na majambazi hao walikataa kujisalimisha na kuwafyatulia risasi polisi.

    Aidha Bw. Nyigesa alisema polisi pia wamekamata silaha mbili kutoka kwa majambazi hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako