• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapanga kuboresha usafiri kwenye Ziwa Victoria kurahisisha biashara

    (GMT+08:00) 2019-07-14 17:34:43

    Rais wa Tanzania John Magufuli amesema mipango inaendelea ya kuboresha usafiri kwenye Ziwa Victoria linalotumiwa na nchi tatu za Tanzania, Uganda na Kenya ili kurahisisha biashara kwenye kanda hiyo.

    Rais Magufuli ameyasema hayo jana wakati anasalimiana na rais wa Uganda Yoweri Museveni aliyekuwa kwenye ziara ya siku moja kijijini kwa rais Magufuli, Chato mkoani Geita, Tanzania. Kwa mujibu wa rais Magufuli serikali sasa inanunua chombo kimoja na kuvifanyia ukarabati vingine vitano ili kuboresha usafiri kwenye ziwa hilo sambamba na kuchochea shughuli za uchumi. Amesisitiza kuwa baada ya hapo watu wa nchi tatu wataweza kuboresha biashara.

    Kwa upande wake rais Museveni amesema ziara yake hiyo binafsi nchini Tanzania imepanda ngazi na kuwa "Hija ya kisiasa" kwa nchi ambayo imeshiriki sana katika harakati za ukombozi. Akiimithilisha Tanzania kama Makka ya harakati za ukombozi wa Afrika, rais Museveni amesema Tanzania imeacha alama isiyofutika katika mapambano ya ukombozi wa bara la Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako