• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNICEF, na washirika wake wazindua mpango wa upatikanaji wa elimu katika Somaliland

    (GMT+08:00) 2019-07-14 17:35:22

    Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF na washirika wake wamezindua mpango wenye thamani ya dola milioni 64 za kimarekani ili kusaidia watoto wa Somaliland, kaskazini mwa Somalia wapate elimu bora.

    Kwa mujibu wa ripoti za UN News, upatikanaji wa elimu katika Somaliland ni mdogo sana, ambapo zaidi ya asilimia 50 ya watoto hawaendi shule, hususan, matarajio ya elimu kwa watoto wa maeneo ya vijijini na watoto waliofikia umri wa kwenda shule wa wakimbizi wa ndani ndio mabaya zaidi. Ripoti hiyo imeongeza kuwa asilimia 26 tu ya watoto wa jamii za vijijini na asilimia 16 ya watoto wa wakimbizi wa ndani ndio walioandikishwa shule za msingi.

    Ukame, ukosefu wa chakula, umasikini na kukosekana kwa usawa ndio baadhi ya changamoto zinazozuia juhudi za kufanya watoto na vijana wa Somaliland waende shule.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako