• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yafikiria kuchukua hatua zaidi kumaliza ujangili

    (GMT+08:00) 2019-07-15 09:33:33

    Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini Tanzania imekihimiza Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori cha Pasiansi kutoa mafunzo mapya ya ujuzi na mbinu za kuzuia ujangili.

    Naibu mkurugenzi wa idara ya kupambana na ujangili iliyo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania Bw. Robert Mande amesema, mtaala wa masomo katika chuo hicho unapaswa kutoa mbinu mpya kwa wanafunzi ili kuwawezesha kupambana na ujangili kwa ufanisi zaidi.

    Bw. Mande pia amesema, ujangili na biashara haramu ya mimea na wanyamapori imeendelea kuliondolea taifa la Tanzania rasilimali zake za thamani ambazo ni vyanzo endelevu vya pato la serikali ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako