• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Kenya yendeleza rekodi yake nzuri

    (GMT+08:00) 2019-07-15 09:36:10
    Kenya imeendeleza rekodi yake nzuri dhidi ya Brazil katika raga ya wachezaji 15 kila upande hadi ushindi tatu baada ya timu yake ya chipukizi almaarufu Chipu kushinda mechi ya Kundi A 26-24 kwenye michuano ya raga ya dunia ya daraja ya pili ya Under-20 mjini Sao Paulo.

    Japan inaongoza kwa alama 10, nne mbele ya Uruguay nayo Kenya imevuna nne. Brazil iko mkiani kwa alama mbili.

    Ureno na Tonga wako sako kwa bako kwa alama 10 kila mmoja kileleni mwa Kundi B baada ya kuzoa ushindi mbili kila mmoja. Canada ina alama mbili nayo Hong Kong haina kitu. Mashindano haya yatakamilika Julai 21, huku bingwa akipandishwa ngazi kushiriki Raga ya Dunia ya daraja ya juu kujaza nafasi ya Scotland iliyotemwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako