• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe na Zambia kuanzisha mazungumzo kuhusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme

    (GMT+08:00) 2019-07-15 09:37:06

    Kampuni moja ya ubia kati ya wachina na wamarekani inatarajiwa kufanya mazungumzo na serikali za Zimbabwe na Zambia kuhusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa megawati 2,400 katika mto Zambezi.

    Mto huo uko mpakani kati ya nchi hizo mbili zinazokabiliwa na tatizo kubwa la umeme, hususan nchini zimbabwe, ambako watu na viwanda vinakosa umeme kwa saa 18 kila siku.

    Gazeti la Sunday Mail la Zimbabwe limeripoti kuwa, kampuni hiyo imeshinda zabuni ya ujenzi wa mradi huo wenye thamani ya dola bilioni kadhaa za kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako