• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikosi vinavyounga mkono serikali vyazima shambulizi la waasi wa Houthi, Yemen

    (GMT+08:00) 2019-07-15 09:37:38

    Vikosi vinavyounga mkono serikali ya Yemen vimesema, waasi 13 wa Houthi wameuawa walipotaka kushambulia kambi za jeshi la serikali katika mkoa wa kusini wa Dhalea.

    Taarifa iliyotolewa na tovuti ya wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imesema, waasi wa Houthi walizidiwa na kurudi kwenye makao yao yaliyo karibu na mkoa wa kati wa Ibb baada ya kupambana na wanajeshi wa serikali kwa muda mfupi. Taarifa hiyo haikueleza vifo na majeruhi ya vikosi vinavyounga mkono serikali.

    Mwezi Aprili, wapiganaji wa Houthi walifanya mashambulizi kadhaa dhidi ya kambi za vikosi vya serikali, na kufanikiwa kukalia sehemu ya Al Husha magharibi mwa mkoa wa Dhalea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako