• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu watoa wito wa misaada zaidi kwa ajili ya wakimbizi wa Syria walioko nchini Jordan

    (GMT+08:00) 2019-07-15 09:39:53

    Wataalamu wametoa wito wa kuongeza misaada kwa Jordan, ambayo hadi sasa imepata chini ya asilimia 6 ya mahitaji ya misaada kwa ajili ya wakimbizi wa Syria walioko nchini humo.

    Mwanauchumi Bw. Wajdi Makhamreh ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, Jordan imeonesha ukarimu mkubwa kwa kuwapa huduma wakimbizi wa Syria, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kutimiza ahadi yake ya kuisaidia Jordan, kwani kupungua kwa misaada kutaathiri kiwango cha huduma kwa wakimbizi.

    Mwanauchumi mwingine Hosam Ayesh ametoa wito wa kuiunga mkono zaidi Jordan ambayo imepokea wakimbizi milioni 1.3 wa Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako