• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yamruhusu waziri wa mambo ya nje wa Iran kwenda makao makuu ya Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2019-07-15 18:58:36

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo amesema, Marekani inamruhusu waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif kufanya ziara katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, lakini vitendo vya Bw. Zarif na ujumbe wake vitakabiliwa na vizuizi.

    Bw. Pompeo amesema kutoa visa kwa Bw. Zarif kufanya ziara huko New York kunategemea wajibu wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa. Lakini amesisitiza kuwa vitendo vya Bw. Zarif na ujumbe wake vinahuzu safari za kwenda na kurudi kati ya makao makuu ya Umoja huo, ofisi ya ujumbe wa Iran katika Umoja wa Mataifa na ofisi ya mjumbe wa kudumu wa Iran katika Umoja huo.

    Rais Hassan Rouhani wa Iran leo mapema ametoa hotuba akisema, kama Marekani itaondoa vikwazo dhidi ya Iran na kurudi katika makubaliano ya suala la nyuklia la Iran, Iran itapenda kufanya mazungumzo na Marekani. Bw. Pompeo amesema, rais Donald Trump wa Marekani atafanya uamuzi wa mwisho, huku akisema makubaliano ya suala la nyuklia la Iran yaliyofikiwa na serikali ya Obama ni janga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako