• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 10 nchini Nigeria kwenye shambulizi lililotokea wikiendi hii

    (GMT+08:00) 2019-07-15 19:10:59

    Miili ya watu 10 imepatikana kwenye kijiji kilichoshambuliwa na watu wenye silaha wikiendi iliyopita katika jimbo la Katsina, nchini Nigeria. Watu wenye silaha walimvamia kijiji cha Kirtawa na kuwaua watu hao na kuwajeruhi wengine watano, ikiwa ni pamoja na wana usalama.

    Watu wenye silaha zaidi ya 300 wakiwa kwenye pikipiki walimvamia kijiji, na kuleta taharuki. Wenyewe wamesema washambuliaji hao pia waliua mifugo kadhaa kabla ya kutokomeza maporini.

    Tukio hilo lililotokea jumamosi ni tukio shambulizi la karibu zaidi kutokea katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria ambako mashambulizi ya ujambazi na wizi wa mifugo yanatokea mara kwa mara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako