• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia mmoja wa China aporwa na kuuawa Ethiopia

    (GMT+08:00) 2019-07-15 19:40:24

    Habari kutoka ubalozi wa China nchini Ethiopia zinasema raia saba wa China jana waliporwa na majambazi wenye visu katika jimbo la Oromia, na mmoja kati yao ameuawa.

    Tukio hilo lilitokea karibu na eneo la viwanda lililojengwa na kampuni ya China jimboni Oromia, ambalo liko umbali wa kilomita 100 kutoka mji mkuu wa Addis Ababa. Raia saba wa China ni wafanyakazi wa eneo hilo la viwanda.

    Ubalozi wa China nchini Ethiopia umetoa mwito kwa Ethiopia kuwafikisha majambazi hao mbele ya sheria haraka iwezekanavyo na kuwaadhibu vikali, na kuzitaka pande husika za Ethiopia zilinde usalama wa uhai na fedha pamoja na haki halali za makampuni, mashirika na raia wa China nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako