• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madereva kulipa zaidi kwa mafuta ya petroli, na kidogo kwa mafuta ya dizeli, mafuta taa

    (GMT+08:00) 2019-07-15 19:56:43

    Madereva wa Kenya wataanza kulipa zaidi kwa mafuta baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Mafuta ya Petroli iliongeza bei ya mafuta ya Super Petrol na Sh0.29 nas itauzwa kwa Sh115.39 kwa lita kwa mwezi mmoja.

    Hata hivyo wanunuzi wa mafuta ya Dizeli na taa imeshuka chini na sh 0.88 na sh 2.31 kwa lita bei ya rejareja ni Sh103.88 na Sh101.97 kwa mtiririko huo.

    Kwa mujibu wa Mamlaka, bei ni imetokana na gharama za wastani za mafuta ya petroli iliyoagizwa kupungua kwa asilimia 1.83 kutoka kwa dola 538.08 kwa kila mita ya ujazo mwezi Mei 2019 hadi dola za Marekani 528.26 kwa mita za ujazo mwezi Juni 2019.

    Mombasa, petroli itanunuliwa kwa Sh112.74, dizeli Sh101.25 na mafuta taa Sh99.35 kwa lita.

    Nakuru petroli Sh115.86, dizeli Sh104.58 kwa dizeli na mafuta taa Sh102.69 kwa lita.

    Eldoret, 116.86, dizeli Sh105.59 na mafuta ya taa Sh103.68.

    Kisumu Sh116, dizeli Sh105.58 na mafuta taa Sh103.67 kwa lita.

    Bei ya mafuta ya petroli imekuwa ikipanda juu katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako