• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Kocha wa Cheka amtetea Mwakinyo

    (GMT+08:00) 2019-07-16 07:57:53
    Licha ya wadau wa ngumi nchini Tanzania kujiuliza maswali juu ya mwenendo wa bondia Hassan Mwakinyo kwenye mchezo huo wa ngumi ama ndondi ama masumbwi, kocha wa bondia Francis Cheka, Abdallah Saleh amemkingia kifua.

    Mwakinyo baada ya kumchapa Sam Eggington aliyekuwa bondia namba nane wa dunia kwenye uzani wa welter kwa TKO, septemba 8 mwaka jana pambano lililoacha gumzo nchini Uingereza, amekuwa akipigana na mabondia ambao baadhi ya wadau wa ngumi wamedai ni dhaifu kulinganisha na rekodi yake.

    Saleh amesema, kila bondia anapaswa kujipa muda wa kupumzika kati ya pambano na pambano, na kwa mwaka bondia anapaswa kuchezo mapambano matatu ama manne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako