• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wa usalama na watunga sera kutoka Afrika Mashariki watoa wito wa kuongeza juhudi za pamoja katika kutatua migogoro

    (GMT+08:00) 2019-07-16 09:06:50

    Wataalam wa usalama na watunga sera kutoka Afrika mashariki wamesisitiza haja ya kuongeza kasi ya juhudi za upatanishi ili kuunganisha mafanikio yaliyofikiwa katika suluhisho la amani la migogoro katika kanda hiyo.

    Wito huo umetolewa wakati wa mkutano wa siku tatu wa kikanda ulioanza jana mjini Addis Ababa, Ethiopia, uliowakutanisha wataalam wa usalama na watunga sera kutoka nchi wanachama wa Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki (IGAD).

    Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Amani ya Shirika hilo Bw. Siraj Fegesa amesisitiza tena ahadi ya IGAD katika kuimarisha suluhisho la kiujenzi la migogoro katika eneo hilo. Amesema ni wazi kuwa mchakato wa amani unaweza kutimizwa kupitia majadiliano na mazungumzo, kama njia ya kutatua migogoro na kuleta amani ya kudumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako