• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yahimizwa kuongeza ushirikiano na China katika sekta nyingine zaidi ya miundombinu

    (GMT+08:00) 2019-07-16 09:10:04

    Mtaalam wa uchumi kutoka Zambia Bw. Misheck Mwanza amesema, kushirikisha wachina katika ujenzi wa sekta ya viwanda nchini Zambia ni njia inayopaswa kuzingitiwa katika siku zijazo, na pia ni njia bora ya kuimarisha uhusiano kati ya China na Zambia ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 55.

    Bw. Mwanza aliyekuwa mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Kidiplomasia na Mambo ya Kimataifa ya Zambia amesema, Zambia inapaswa kuhamasisha uwekezaji zaidi wa China katika sekta ya uzalishaji.

    Amesema katika miaka ya hivi karibuni miradi mingi ya ushirikiano kati ya Zambia na China imekuwa katika maendeleo ya ujenzi wa miundombinu, lakini Zambia inapaswa kushirikisha China katika uwekezaji katika sekta ya viwanda, ili kutoa ajira na kuongeza kipato cha wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako