• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ndogo ya viwanda vya utengenezaji vya China vinahamia katika nchi za nje

    (GMT+08:00) 2019-07-16 17:06:04

    Msemaji wa Kamati ya maendeleo ya Mageuzi ya China Bibi Meng Wei amesema, ni idadi ndogo ya viwanda vya utengenezaji vya China vinavyohamia nchi za nje, na vingi kati yao ni vya ngazi vya chini na vya kati. Amesema athari ya vianda hivyo kwa ongezeko la uchumi, kupanda kwa ngazi ya viwanda, na upatikanaji wa ajira nchini China inaweza kudhibitiwa.

    Akizungumzia ripoti kuhusu viwanda vya China hususan vile vya utengenezaji vinavyohamia nje ya nchi ambavyo vilionekana hivi karibuni katika baadhi ya vyombo vya habari, Bibi Meng Wei amesema, inapaswa kuchukua ripoti kama hizo kwa msimamo wa kimantiki.

    Bibi Meng Wei amesema, tangu sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ianze kutekelezwa, maendeleo ya viwanda vya utengenezaji vya China yamepata mafanikio makubwa, na kuuza bidhaa zenye sifa bora na bei nafuu kwa nchi mbalimbali duniani, pia kutoa soko kubwa kwa viwanda vya nchi mbalimbali duniani. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na marekebisho ya kina kuhusu mgawanyiko wa viwanda vya kimataifa na muundo wa viwanda duniani, viwanda vya utengenezaji vya China vimeingia katika kipindi kipya cha kubadilika na kupanda ngazi, na kuelekea kupata maendeleo yenye sifa bora. Katika mchakato huo, baadhi ya viwanda kuhamia mnyororo wa utengenezaji katika nchi za nje ni hali ya kawaida. Bibi Meng anasema:

    "Kati ya viwanda kama hivyo vinafikiria mabadiliko ya bei, na kuhamia katika sehemu zenye ghamara ndogo za uzalishaji. Baadhi ya viwanda hivyo vinafanya juhudi za kupanua soko la kimataifa kutokana na mahitaji yao ya mkakati wa kujiendeleza. Na vingine vichache vinataka kujiepusha na athari kutokana na mgogoro ya biashara kati ya China na Marekani."

    Bibi Meng Wei ameelezea kuwa, si jambo rahisi kwa viwanda kuhamia katika nchi za nje, na kwamba vinapaswa kufikiria hali mbalimbali zikiwemo gharama za uendeshaji, wafanyakazi wa viwanda, mnyororo wa utoaji wa bidhaa pamoja na mawasiliano, uchukuzi hata utamaduni wa viwanda vya utengenezaji. Anasema:

    "Katika miaka ya hivi karibuni vilevile tumegundua kuwa, baadhi ya viwanda ambavyo vilihamia katika nchi za nje vimerudi nchini kutokana na kutozoea mazingira ya huko. Kutokana na hali tunayofahamu, idadi ya viwanda vya utengenezaji ya vinavyohamia katika nchi za nje si kubwa, na pia vinahusisha zaidi viwanda vya ngazi vya kati na vya chini, na athari zinazoletwa kutokana na hali hii zinaweza kudhibitiwa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako