• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pakistan yafungua eneo lake la anga kwa usafiri wa ndege za kiraia

    (GMT+08:00) 2019-07-16 17:57:53

    Idara ya usimamizi wa usafiri wa ndege za kiraia ya Pakistan imetangaza kuwa eneo la anga la nchi hiyo limefunguliwa tena kwa usafiri wa ndege za kiraia za aina zote.

    Mwezi wa Februari mwaka huu, Pakistan na India zilipambana katika sehemu ya Kashmir, na ndege za kivita za pande mbili ziliingia katika eneo la sehemu ya Kashmir lililodhibitiwa na upande mwingine. Idara ya usimamizi wa usafiri wa ndege za kiara za Pakistan ilitangaza Februari 26 kufunga kwa muda eneo lake la anga, hivyo mashirika kadhaa ya safari za ndege ya kimataifa yaliathiriwa na kusimamisha au kufuta safari za ndege kupitia eneo la anga la Pakistan. Mwezi wa Machi baadhi ya maeneo yake ya anga yalifunguliwa, lakini ndege za India na Afghanistan hazikuruhusiwa kuingia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako