• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema hoja ya Marekani kuhusu uchumi wa China ni upotoshaji mtupu

    (GMT+08:00) 2019-07-16 19:44:32

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, hoja ya Marekani kwamba China inataka sana kufikia makubaliano nayo kutokana na kupungua kwa kasi ya ongezeko la uchumi ni upotoshaji mtupu.

    Rais Donald Trump wa Marekani ametoa taarifa kupitia mtandao wa kijamii ikisema, kasi ya ongezeko la uchumi wa China katika robo ya pili ya mwaka huu iko chini zaidi katika miaka 27 iliyopita. Maelfu ya mashirika yanaondoka China, hivyo China inataka sana kufikia makubaliano ya kibiashara na Marekani.

    Bw. Geng amesema, katika hali ambayo kasi ya ongezeko la uchumi wa dunia inapungua na mambo ya nje yasiyo na uhakika yanaongezeka, ongezeko la pato la taifa la China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu limefikia asilimia 6.3, ambalo linaongoza katika makundi makuu ya kiuchumi duniani.

    Pia amesema kufikia makubaliano ya kibiashara si matakwa ya upande mmoja wa China. Watu wa nyanja mbalimbali na wateja wengi nchini Marekani, pia wanapinga kuongeza ushuru dhidi ya China na kupinga kithabiti vita vya kibiashara. Sauti hizo ni uthibitisho wenye nguvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako