Jukwaa hili la biashara linaandaliwa na Shirikisho la Sekta Binafsi Rwanda chini ya kaulimbiu ya "Kufungua Biashara ya Afrika,Yenyewe ,na Ulimwengu" kama kongamano la kila mwaka ambalo linawaleta pamoja wadau mbalimbali kujadiliana,kugundua fursa,na kubadilishana uzoefu wa namna uchumi unaosukumwa na sekta binafsi unaweza kuwa na ufanisi.
Mkutano huo utaleta pamoja washiriki takriban 1000 kutoka Afrika,Asia,Ulaya,na Amerika.
Mada zitakazojadiliwa ni pamoja na faida ya ushindani wa bara la Afrika-soko moja kubwa na mkataba wa biashara huru,na hali ya uzoefu wa kibiashara wa Afrika na China na jinsi China ilivyojiimarisha kufanya biashara na Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |