• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pamba yote ya Tanzania kununuliwa ifikapo Julai 30,asema Waziri Mkuu Majaliwa

    (GMT+08:00) 2019-07-16 20:17:20
    Kufikia tarehe 30 Julai mwaka huu,pamba yote iliyoko mikoa mbalimbali nchini Tanzania itakuwa imeshanunuliwa na wakulima kulipwa fedha zao.

    Hayo ni kwa mujibu wa Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,ambaye alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mbutu na Mwabakima alipokuwa katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Igunga mkoani tabora.

    Alisema serikali imeamua kuingilia kati sula la ununuzi wa zao la pamba kutokana na kudorora kwa soko lake ,kwa kutoa dhamana ili kuwawezesha wanunuzi kukopeshwa fedha na benki mbalimbali kwa ajili ya kununulia pamba kutoka kwa wakulima.

    Hivyo,aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya katika maeneo yote yanayolima zao hilo wawasimamie ipasavyo wanunuzi wote ili kuhakikisha fedha zitakazopatikana zinakwenda kutumika kwa ajili ya kununulia pamba na si vinginevyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako