• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Dortmund waelekea Marekani kwa kambi ya mazoezi

    (GMT+08:00) 2019-07-17 08:17:50
    Borrusia Dortmund wameondoka juzi kwenda Marekani kwa ajili ya ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya. BVB wanasafariri bila ya beki wao wa kati Abdou Diallo ambaye anahusishwa na uhamisho wa kujiunga na mabingwa wa Ufaransa Paris Saint-Germain.

    Msemaji wa klabu hiyo amethibitisha habari hizo, na kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, Diallo tayari yuko Paris kwa ajili ya vipimo vya matibabu.

    BVB watakuwa Marekani kwa wiki moja ambapo watacheza na Seattle Sounders Alhamisi na kisha mabingwa wa Champions League Liverpool wanaoongozwa na kocha wa zamani wa Dortmund Juergen Klopp siku ya Jumamosi. Msimu wa Bundesliga unaanza katikati ya Agosti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako