• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani haitauza ndege za F-35 kwa Uturuki baada ya mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa Russia S-400 kufika

    (GMT+08:00) 2019-07-17 09:24:48

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema serikali yake haitauza ndege za kivita za F-35 kwa Uturuki kwa sababu nchi hiyo imenunua mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora angani wa Russia S-400. Pia ameikosoa serikali ya awamu iliyopita kwa kukataa kuuza mifumo ya Patriot ya Marekani na kusababisha makubaliano hayo kati ya Uturuki na Russia. Wizara ya ulinzi ya Marekani pia imekataa kauli inayosema kuwa Uturuki ilinunua mfumo wa S-400 baada ya kushindwa kupata mfumo huo, na kusema Marekani imezungumza na Uturuki mara nyingi kuhusu mfumo wa Patriot lakini Uturuki haikusaini mkataba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako