• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa msaada wa mchele kwa ajili ya wanafunzi wa Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2019-07-17 09:40:51

    Serikali ya China imekabidhi msaada wa tani 2,185 za mchele kwa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, ili kuchangia mradi wa kuwapatia chakula wanafunzi wa shule nchini Sudan Kusini.

    Naibu mkuu wa ofisi ya shirika hilo nchini Sudan Kusini Bw. Steve Nsubuga amesema, msaada huo utatumiwa kuwapatia chakula wanafunzi 86,000 wa shule 230 nchini humo.

    Kaimu balozi wa China nchini Sudan Kusini Bw. Liu Xiaodong amesema, msaada huo ni sehemu ya juhudi za China katika kuisaidia Sudan Kusini kuimarisha usalama wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako