• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zatarajia kuimarisha ushirikiano wa kiusalama na China

    (GMT+08:00) 2019-07-17 10:38:58

    Kongamano la Amani na Usalama kati ya China na Afrika linaendelea hapa Beijing, ambapo maofisa waandamizi karibu 100 kutoka nchi 50 za Afrika na idara ya ulinzi ya Umoja wa Afrika pamoja na wajumbe wa jeshi la China wanajadili jinsi ya kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika mambo ya amani na usalama.

    Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia Amani na Usalama Bw. Smail Chergui amesema, ugaidi ni changamoto kubwa zaidi inayolikabili bara la Afrika, na China ni mwenzi muhimu wa ushirikiano wa Afrika, hivyo Umoja wa Afrika unapenda kuimarisha ushirikiano na China katika sekta ya usalama.

    Waziri wa ulinzi wa Mauritania Yahya Ould Hademine ameishukuru China kwa kuandaa kongamano hilo, na kusema dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa na juhudi za China na Afrika kushirikiana katika kuimarisha usalama zinasaidia watu wa Afrika kupata haki na usawa.

    Anasema, "Kama tujuavyo, China inajitahidi kujenga uhusiano wenye usawa na nchi nyingine, lakini nchi za magharibi zinatoa masharti mengi katika kushirikiana na nchi za Afrika katika mambo ya usalama. Ushirikiano na China unanufaisha pande zote. Naona China inafanya kazi muhimu katika kulinda amani na usalama, kwani ina ushawishi mkubwa duniani katika sekta za uchumi na jeshi."

    Waziri wa ulinzi wa Benin Alain Fortunet Nouatin amesema ushirikiano wa kiusalama kati ya China na Afrika una historia ndefu, na unaendelezwa vizuri. Pande hizo mbili zimefanya ushirikiano katika mambo mbalimbali kama vile kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa kigeni wanaosomea mambo ya jeshi, na kutoa misaada ya mbinu za kivita na vifaa vya kijeshi. Ameeleza matumaini yake kuwa China na Afrika zitaweza kuimarisha zaidi ushirikiano wao katika sekta nyingine. Anasema, "Kwanza sekta tunazoweza kufanyia ushirikiano bado ni nyingi, kwa mfano katika mbinu za kivita zinazotumia teknolojia ya habari, kukusanya taarifa zinazotishia usalama wa taifa ili kuchukua hatua za tahadhari. Pili, China inaweza kutoa msaada zaidi katika vifaa vya kijeshi. Tatu ni kuwa China inatarajiwa kutoa msaada na ulinzi katika usalama wa baharini kama vile kulinda usafiri baharini, usalama wa usafirishaji bidhaa, haswa usalama wa Ghuba ya Guinea."

    Naibu mnadhimu mkuu wa kikosi cha usalama cha Sierra Leone Taluva David Tamba Ocil amesema, baadhi ya mashirika ya kimataifa huwa yanatoa wito kwa nchi za Afrika kupunguza matumizi katika ulinzi wa kitaifa na kupunguza idadi ya wanajeshi ili kupunguza matumizi ya serikali, lakini nchi za Afrika zinapokabiliwa na matishio ya kiusalama, haziwezi kupata msaada. Anatarajia kuwa nchi za Afrika na China zinaweza kuongeza ushirikiano katika ujenzi wa ulinzi wa kitaifa ili kulinda maslahi ya nchi hizo na kuboresha maisha ya watu. Anasema, "Baadhi ya nchi hazina uwezo wa kimsingi wa ulinzi wa kitaifa kulinda mamlaka na maliasili mbalimbali, hali hii inafanya nchi maskini zizidi kuwa maskini. Baadhi ya nchi zina fukwe ndefu lakini zinashindwa kukabiliana na wavamizi kutoka nje. Pia kuna baadhi ya nchi za Afrika hazina vifaa vya ulinzi wa mtandao wa internet na hivyo kushindwa kukabiliana na changamoto za kigaidi. Kama China inaweza kusaidia nchi za Afrika kuongeza uwezo wa ulinzi wa kitaifa, kulinda maliasili na kuhimiza maendeleo ya taifa, itakuwa na manufaa makubwa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako