Nchi zilizo kwenye kanda ya Maziwa Makuu zimeahidi kuongeza uwazi katika mchakato wa uchaguzi ili kuimarisha amani, utulivu, ujumuishi na maendeleo endelevu.
Wabunge na wataalam kutoka kanda hiyo wamesema katika mkutano wao uliofanyika Nairobi, Kenya, kuwa kuboresha usimamizi wa uchaguzi ni ufunguo wa kuzuia vurugu ambazo zinatishia mshikamano na maendeleo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Bi. Monica Juma amesema, chaguzi zinazofanyika kwa uhuru, usawa na uwazi ni hitaji muhimu la kudumisha utulivu, amani na maafikiano katika kanda ya Maziwa Makuu.
Amesema kuboresha mchakato wa uchaguzi katika kanda hiyo kupitia matumizi ya teknolojia na ushirikishwaji mkubwa wa wananchi kutaongeza kasi ya ushirikiano kati ya nchi zinazokabiliwa na migogoro ya kisiasa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |