• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la chini la bunge la Marekani lapitisha azimio la kulaani "kauli ya ubaguzi wa rangi" iliyotolewa na Trump

    (GMT+08:00) 2019-07-17 18:56:57

    Baraza la chini la bunge la Marekani limepitisha azimio la kulaani "kauli ya ubaguzi wa rangi" iliyotolewa na rais Trump kwa kura 240 za ndiyo dhidi ya kura 187 za hapana.

    Azimio hilo limesema "Kauli ya ubaguzi wa rangi iliyotolewa na rais Donald Trump wa Marekani inalaaniwa vikali, kauli ambayo inahalalisha na kuchochesha hofu na ugomvi dhidi ya wahamiaji nchini Marekani na watu wasio wazungu."

    Rais Trump alitoa kauli kupitia akaunti ya Twitter tarehe 14 mwezi huu akisema wabunge wa kike wa kamati moja ya Chama cha Kidemokrasia wanatakiwa "kurudi makwao kulikojaa umaskini na uhalifu" badala ya kuingilia utawala wa nchi ya Marekani, ambao wanawake hao wanne waliotajwa wote ni Wamarekani wasio wazungu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako