• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inatarajia Marekani kuonesha nia thabiti kwa kufikia makubaliano ya uchumi na biashara ya kunufaishana

    (GMT+08:00) 2019-07-17 19:37:31

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Geng Shuang, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa China siku zote inasisitiza kutatua mgogoro wa kiuchumi na kibiashara kati yake kwa njia ya mazungumzo, pia ina udhati kwa mazungumzo ya uchumi na biashara. Vilevile amesema China inatarajia Marekani ioneshe nia thabiti kwa kufikia makubaliano ya uchumi na biashara ya kunufaishana kwa kushirikiana na China chini ya msingi wa kuheshimiana na kutendeana kwa usawa.

    Bw. Geng akijibu kuhusu kutekeleza sheria ya Marekani ya kuendelea kuweka vikwazo dhidi ya kampuni ya Huawei, amesema wabunge husika wa Marekani wamezuia maendeleo ya China, kuvuruga uhusiano kati ya China na Marekani, kuzishinikiza kampuni za China bila sababu, na pia kuathiri maslahi ya kampuni za Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako