• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China atoa wito kuunda mazingira ya amani na utulivu kwa vijana

    (GMT+08:00) 2019-07-18 19:25:16

    Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatakiwa kuimarisha kutatua masuala ya kikanda kwa njia ya kisiasa, na kuweka mazingira ya amani na utulivu kwa vijana.

    Bw. Wu amesema hayo kwenye mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya vijana, amani na usalama, akiongeza kuwa baraza hilo linatakiwa kukinga na kutatua migogoro kwa njia ya kisiasa, kuzisaidia nchi husika zinazokumbwa na migogoro kuhimiza mchakato wa amani, kuzuia mateso ya ugaidi na msimamo mkali kwa vijana.

    Bw. Wu amesisitiza kuwa chanzo kikuu cha migogoro ni umaskini na maendeleo yasiyo na uwiano, na Umoja wa Mataifa unatakiwa kusaidia nchi zinazoendelea kuongeza uwezo wa kuwa na maendeleo endelevu, na kuhimiza kutekeleza ajenda za maendeleo endelevu za mwaka 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako