• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • URA yapitisha malengo ya ukusanyaji ushuru

    (GMT+08:00) 2019-07-19 07:50:43

    Katika mwaka wa fedha 2018/2019 uchumi wa Uganda umekua kwa asilimia 6.1 dhidi ya matarajio ya ukuaji wa asilimia 6.

    Kamishana Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Uganda,Bi Doris Akol anasema ukuaji huo wa uchumi ni chachu ya ufwatiliaji na ulipaji ushuru.

    Wakati akitoa Ripoti ya utendaji wa uchumi chini ya kaulimbiu ya "uwazi na uwajibikaji kwa utoaji huduma bora",Bi Akol alisema kuwa vyanzo vikuu vilivyochangia ukusaji wa mapato viliandikisha ukuaji chanya wakati wa mwaka wa kifedha,na kusema kuwa sekta ya uchimbaji madini iliandikisha ukuaji wa asilimia 17.6,biashara asilimia 6.6,na ujenzi asilimia 5.7.

    Nyengine ni pamoja na viwanda,asilimia 4.4,fedha na bima asilimia 8.3 na utawala wa umma asilimia 10.6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako