• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa Umoja wa Ulaya washindwa kuafikiana kuhusu tatizo la watu wanaotafuta hifadhi katika eneo la Mediterranean

    (GMT+08:00) 2019-07-19 09:09:18

    Mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Helsinki, Finland, wameshindwa kufikia makubaliano ya jinsi ya kukabiliana kwa pamoja na mgogoro wa wahamiaji katika eneo la Mediterranian.

    Waziri wa mambo ya ndani wa Finland Bi. Maria Ohisalo amesema, nchi yake inaendelea kufanya kazi kwa ajili ya kuchukua wajibu mkubwa zaidi katika kuwapatia makazi watu wanaotafuta hifadhi. Ameongeza kuwa, mazungumzo yanaonyesha kwamba nchi wanachama wana lengo la wazi la kuendeleza mfumo wa Ulaya kwa watu wanaotafuta hifadhi, licha ya changamoto zilizopo.

    Kamishna wa Uhamiaji, masuala ya ndani na uraia wa Umoja wa Ulaya Bw. Dimtris Avramopolous amesema, uamuzi wa kushughulikia suala hilo bado haujafikiwa, lakini hakuwa tayari kuzungumzia zaidi suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako