• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China atoa wito wa kuendeleza ujenzi wa uwezo katika nchi zilizokuwa na vita

    (GMT+08:00) 2019-07-19 09:09:38

    Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Wu Haitao amesema, jamii ya kimataifa inapaswa kutilia maanani ujenzi wa uwezo katika nchi ambazo zimesimamisha mapigano ili nchi hizo zipate maendeleo ya kujitegemea.

    Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja huu kuhusu kuimarisha uhusiano kwa ajili ya mafanikio ya mpito wa nchi husika, balozi Wu amesema Umoja wa Mataifa na wenzi wengine unapaswa kufuata nia na kanuni za Mkataba wa Umoja huo, na kuheshimu mamlaka na utaifa na kutoa msaada wa kiujenzi kutokana na matakwa ya nchi husika.

    Amesema nchi nyingi baada ya vita kumalizika, zimeanza ujenzi wa nchi zao na ziko kwenye awamu ya mpito ya ujenzi wa Amani na maendeleo ya muda mrefu, hivyo Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa zinapaswa kutoa msaada wa kiujenzi na kuziunga mkono nchi husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako