• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waadhimisha Siku ya kimataifa ya Nelson Mandela

    (GMT+08:00) 2019-07-19 19:00:21

    Baraza kuu la 73 la Umoja wa Mataifa limefanya mkutano wa kuadhimisha "Siku ya kimataifa ya Nelson Mandela" kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini New York.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amehutubia mkutano huo akitoa wito wa kurithi matumaini ya Bw. Mandela ambayo bado hayajatimizwa, na kulinda kanuni na msimamo wa thamani wa katiba ya Umoja wa Mataifa. Amesema huu ni mwaka wa kwanza wa "Miaka kumi ya amani ya Nelson Mandela (2019-2028)". Hata hivyo, hivi sasa migogoro mingi bado inaendelea na hakuna dalili ya kusimamisha, na inaleta shinikizo kubwa kwa mfumo wa utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi. Hivyo, wito wa kujenga dunia yenye amani uliotolewa na Bw. Mandela umekuwa muhimu zaidi hivi leo.

    Wakati huo huo mwenyekiti wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bibi Maria Espinosa ametaka watu wote waondoe tofauti na kushikamana chini ya mwongozo wa moyo wa Bw. Mandela, ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako