• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi kivuko cha Kayenze sasa kukamilika Novemba

    (GMT+08:00) 2019-07-19 21:37:43
    Ujenzi wa kivuko cha Kayenze kwenda Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza unaogharimu Sh. bilioni 2.7 unatarajiwa kukamilika Novemba mwaka huu.

    Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema hayo alipotembelea kivuko hicho kuangalia maendeleo ya ujenzi.

    Kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 250, magari 10 na ukubwa wa tani 10 kitaondoa kero ya muda mrefu waliyokuwa wakiipata wananchi wa Kayenze na Bezi.

    Seikali ya Tanzania imeahidi ujenzi huo utakamilika mapema kulitokana na changamoto kadhaa na mojawapo ni kukwama kwa vifaa bandarini kulikosababishwa na msamaha wa ushuru ambapo hata hivyo. Aidha imeongeza kushughulikia suala hilo na kufafanua kuwa Oktoba mwaka 2019 kivuko hicho kitafanyiwa majaribio rasmi kabla ya kukabidhiwa mwezi mmoja baadaye kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.

    Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni inayotengeneza kivuko hicho ya Songoro Marine Ltd, Meja Songoro, alisema ujenzi wa kivuko hicho ulioanza Januari mwaka huu uko katika hatua za mwisho mwisho na kuwa sasa kampuni yake inakamilisha kufunga mifumo ya maji, umeme, zimamoto, kufunga ingini na vifaa vya kuendeshea kivuko hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako