• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yakosoa makadirio ya benki ya dunia ya ukuaji wa uchumi

    (GMT+08:00) 2019-07-19 21:38:04

    Taasisi ya takwimu nchini Tanzania imesema kuwa inaweza kutathmini takwimu za ukuaji wa uchumi wake wa mwaka 2018 baada ya Benki ya dunia kutoa takwimu zilizoonyesha kiwango cha chini cha ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

    Waziri wa fedha wa Tanzania amesema kuwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kilikuwa ni 7% mwaka jana.

    Benki ya dunia ambayo ilitoa hesabu zake kwa misingi ya data za taifa , matarajio ya mwaka 2019 ya ukuaji wa kiwango cha 5.4% - pia ilitoa kiwango cha chini cha ukuaji chini ya kile kilichokuwa kimekadiriwa na na serikali cha 7.1%. Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ametetea njia zake na namna alivyofikia kiwango hicho.

    Kwa mujibu wa Benki ya Dunia uchumi wa taifa la Tanzania ulikua kwa asilimia 5.2 mwaka 2018. Ukuaji wa mwaka uliopita uliathiriwa na kushuka kwa viwango vya uwezekazaji, mauzo katika mataifa ya kigeni na ukopeshaji katika sekta ya kibinfasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako