• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yasema imekamata meli ya mafuta ya Uingereza ili kulinda "kanuni za bahari"

    (GMT+08:00) 2019-07-21 18:59:04

    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Javad Zarif amesema Iran inaishikilia meli ya mafuta ya Uingereza ili "kulinda kanuni za kimataifa za bahari".

    Bw. Zarif amesema tofauti na uharamia kwenye mlango bahari wa Gibraltar, kitendo cha Iran kwenye ghuba kina lengo la kulinda kanuni za bahari za kimataifa.

    Mapema mwezi huu jeshi la majini la Uingereza liliikamata meli ya Iran kwenye mlango bahari wa Gibraltar, ambayo Uingereza ilisema ilikuwa inaelekea Syria, kitu ambacho ni kinyume na vikwazo vya Umoja wa Ulaya.

    Ijumaa kikosi cha ulinzi wa mapinduzi cha Iran kiliikamata meli ya mafuta ya Uingereza "Stena Impero" kwenye mlango bahari wa Hormuz, kwa kile kilichotajwa kuwa ni kushindwa kuheshimu sheria za bahari za kimataifa wakati inapita hapo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako