• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: uharibifu wa Ndege kugharimu Shirika takriban dola milioni 10

    (GMT+08:00) 2019-07-22 19:53:43
    Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege ya Kenya (KAA) inapanga kutumia karibu Sh bilioni 1 ili kuzuia hatari ya mgomo wa ndege, ambayo imechangia kwa kutua kwa dharura ambayo imegharimu mashirika ya ndege mabilioni ya pesa katika uharibifu wa injini.

    Mpango huo, ni kuzuia viumbe vya mabawa yaani ndege, katika uwanja wa ndege.

    Mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa wanyamapori,bwana George Amutete, amesema mpango huu utanyika kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kisumu, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mombasa.

    Bwana George Amutete amesema wanampango wa kununua chombo ambacho kitatumiwa kuonyesha marubani vitu kwenye skirini kama vile ndege na kadhalika vinavyokaribia eneo lao… maarufu kama rada ili kuzuia mgomo wa viumbe vya mabawa yaani ndege ambayo, ikiwa imewekwa, inaweza kusaidia kuona viumbe hivyo hadi umbali wa maili tano na kuonya marubani mapema.

    Amesema mfumo huo utaweza kupunguza uharibifu unaohusishwa na injini kutoka asilimia 33 ya sasa hadi asilimia tano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako