• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Viongozi wapinga uuzaji wa viwanda vya sukari

    (GMT+08:00) 2019-07-23 18:16:51
    Viongozi kutoka maeneo yanayokuza miwa Magharibi mwa Kenya, wameitaka serikali kusimamisha shughuli za kubinafsisha viwanda vya sukari vilivyoko eneo hilo kutokana na changamoto za usimamizi na fedha.

    Badala yake, viongozi hao wanataka washikadau katika sekta hiyo kujadiliana na kutafuta suluhisho la kudumu kwa kampuni hizo, ili ziendelee kufanya kazi inavyofaa na kuhakikishia wakulima wa miwa kuwa watakuwa na soko la mazao yao na watakuwa wakilipwa muda ufaao.

    Wakiongozwa na seneta wa kaunti ya Bungoma Moses Wetang'ula, viongozi hao walisema kuwa kuharakisha kubinafsisha kampuni hizo kutawasababishia wakulima wa miwa matatizo ya kiuchumi. Gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati aliitahadharisha serikali dhidi ya kuharakisha kubinafsisha viwanda vya sukari na kampuni zingine zilizoko eneo hilo, akiitaka kuachia serikali za kaunti kushiriki katika shughuli hizo kwa niaba ya wananchi.

    Kumekuwa na madai kuwa usimamizi wa kiwanda hicho ulikuwa ukiwalipa watu wengine wanaokiuzia miwa, wakati wakulima wa eneo hilo wanaachwa nje, kwa kuwa wanaolipwa wamekuwa wakitoa hongo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako