• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujumbe wa China wasaka nafasi za kuwekeza Tanzania.

    (GMT+08:00) 2019-07-23 18:17:12
    Ujumbe kutoka Jimbo la Zhejiang nchini China, uko nchini Tanzania kusaka fursa za uwekezaji, pamoja na kukutana na wafanyabiashara mbali mbali, kutoka Tanzania.

    Akizungumza katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam hiyo jana, Mwenyekiti wa ujumbe huo, Ge Huijun, alisema hatua hiyo inatokana na ushirikiano wa China na Tanzania, ambao umezidi kuimarishwa siku za hivi karibuni.

    Alisema jimbo la Zhejiang lenye zaidi ya wakazi milioni 57 lina fursa nyingi za biashara na uwekezaji, lakini pia lina wakazi wengi wenye uwezo wa kuwekeza nje ambao nao wanahitaji kujua fursa zilizopo Tanzania. Aidha, ujumbe huo pia umetambua fursa za utalii zilizopo Tanzania, na tayari kampeni maalum kwa jina Travel to Tanzania imeanzishwa. Kampeni hii ina uwezo wa kuleta watalii takriban milioni saba kwa mwaka nchini Tanzania.

    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, alisema ziara hiyo ya ujumbe maalumu kutoka China itaimarisha upatikanaji wa mitaji ya uwekezaji na uuzaji mazao nje, kwa kuibua soko jipya la wazalishaji kutoka nchini.

    Profesa Kabudi alisema hiyo ni sehemu ya fursa muhimu kwa wazalishaji wa bidhaa za mashambani nchini, ambao sasa wanatakiwa waangalie soko la zaidi ya watu bilioni moja walioko China.

    Alisema Jimbo la Zhejiang ni la nne kwa ukubwa nchini China likiwa na soko la zaidi ya watu milioni 57, likiwa na sifa kuu ya uzalishaji samaki, mchele, chai na hariri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako