• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: URA yarejesha bilioni 62.5 kutoka kwa walaghai.

    (GMT+08:00) 2019-07-23 18:17:33
    Mamlaka ya ukusaji ushuru nchini Uganda URA, imerejesha shilingi bilioni 62.5, pesa za Uganda kutoka kwa wafanyibiashara walaghai, na wanaojihusisha na vitendo vya kimagendo. Akiongea wakati wa kugagua zoezi la ukusanyaji ushuru, kamishena mkuu wa URA Generali Doris Akol alisema kwamba, kupitia vitengo vya uchunguzi katika ofisi ya ukusanyaji ushuru kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019, ilibainika wazi kwamba kuna visa 88 vya ukwepaji wa kulipa ushuru wa takriban shilingi bilioni 62.5, pesa za Uganda. Hata hivyo, kupitia taarifa za ujasusi wahusika walipatikana na mianya yao ya kukwepa kulipa ushuru kuzibwa.

    Serikali imetoa onyo kali kwa wafanyibiashara na mashirika yanayokwepa kulipa ushuru. Wizara ya hazina ya kitaifa imependekeza kufutiliwa mbali kwa leseni za utendakazi za wafanyibiashara na mashirika yote ambayo yamekuwa yakikwepa kulipa ushuru. Takriban shilingi bilioni moja za ushuru zilirejeshwa kutoka kwa kampuni kadhaa zilizokuwa zimehepa kulipa ushuru. Aidha kampuni 2,000 nchini Uganda zinafanyiwa uchunguzi kuhusiana na swala la kutolipa ushuru kwa URA.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako