• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Kigali kuandaa baraza la Golden Business Forum

    (GMT+08:00) 2019-07-23 18:17:52
    Wawekezaji wa kimataiafa na wafanyibiashara mahiri kutoka pembe zote za dunia wanatarajiwa kujumuika pamoja mapema mwezi ujao jijini Kigali, Rwanda, kwenye Baraza la kwanza la Golden Business.

    Baraza hili litakaloandaliwa kwenye ukumbi wa mikutano wa KCC, litajadili kwa kina jinsi sekta za kibinafsi zinaweza kuongeza mchango wake katika swala zima la ustawi wa jamii na uchumi kwa bara zima la Afrika.

    Baraza hili limeandaliwa na shirikisho la wafanyibiashara wa sekta ya kibinafsi amabyo dhamira yake ni Kufungua nafasi za biashara Afrika pamoja na dunia nzima. Hafla hii itatoa nafasi mwafaka kwa wahusika kujadiliana maswala mablimbali muhimu ya biashara, kutafuta nafasi za biashara, kujipanga, kutetea haki za wafanyibiashara na kushiriki uzoefu wao katika maswala ya biashara, kikanda, barani na ulimwenguni. Zaidi ya washirika 1000 kutoka Afrika, Asia, Uropa na Amerika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako