• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya Umoja wa Mataifa yatangaza Mpango wa hewa safi kabla ya mkutano wa kilele kuhusu hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2019-07-24 10:17:57

    Mashirika ya Umoja wa Mataifa jana yametangaza Mpango wa Hewa Safi, ikiwa ni siku chache kabla ya mkutano wa kilele wa mwaka 2019 kuhusu hali ya hewa, ambao umezitaka serikali za nchi mbalimbali kujitahidi kuhakikisha hali ya hewa inakuwa salama kwa wananchi wao.

    Umoja wa Mataifa, Shirika la Afya Duniani WHO, Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na Muungano wa hali ya hewa na hewa safi, zimezitaka serikali za nchi mbalimbali kushiriki kwa pande zote kwenye mpango huo, na kuendana na sera kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na uchafuzi wa hewa ifikapo mwaka 2030.

    Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mkutano wa kilele wa hali ya hewa Luis Alfonso de Alba amesema, msukosuko wa hali ya hewa na msukosuko wa hewa chafu zinasababishwa na vyanzo vinavyofanana, na vinapaswa kutatuliwa kwa vitendo vya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako