• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni za sukari zakosolewa kwa kususia maonyesho ya kilimo na biashara ya Kisumu

    (GMT+08:00) 2019-07-24 19:14:40

    Wadau wa sekta ya sukari nchini Kenya Kenya wamelalamikia kukosekana kwa kampuni za sukari kwenye maonyesho ya kilimo na biashara mjini Kisumu. Baadhi yao wamesema kitendo hicho kinahujumu juhudi za serikali za kufufua sekta ya sukari nchini Kenya.Kwa miaka mingi kampuni za sukari zimekuwa zikishiriki kwenye maonyesho hayo ya kilimo.Kampuni hizo ambazo zinadaiwa kukosa kushiriki kwenye maonyesho hayo ni pamoja na Transmara , Sukai Industries, Kobos, Muhoroni, na Chemelil. Kampuni ya Sukari ya Sony ambayo awali ilikuwa imeahidi kushiriki kwenye maonesho hayo ilikuwa imelipia kibanda chake lakini lakini hawakuonekana kwenye maonesho hayo. Waandalizi ya maonyesho hayo wamesema wamekabidhi vibanda hivyo kwa kampuni zingine. Naibu mwenyekiti wa maonesho hayoa Bwana

    Morris Roche amesema zaidi ya kampuni 80 zilishiriki kwenye maonesho hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako