• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NEMC yataka kusitishwa kwa bwawa la kuhifadhia tope sumu katika mgodi wa Acasia

    (GMT+08:00) 2019-07-24 19:16:22

    Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini Tanzania limesitisha matumizi ya bwawa la kuhifadhia tope sumu katika Mgodi wa Acacia North Mara baada ya sampuli mbalimbali za vipimo kuonyesha kuwa bado kuna utiririshaji wa maji yenye kemikali sumu. Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Mhandisi Dk. Samuel Gwamaka, amesema kampuni imeshindwa kudhibiti utiririshaji wa maji hayo yenye kemikali za sumu zinazototililika kuelekea katika makazi ya wananchi na kuathiri mazingira pia.

    Dk. Gwamaka amesema NEMC haitamwonea aibu wala huruma mtu au kampuni yoyote inayofanya shughuli zake bila kufuata kanuni na taratibu za kimazingira.

    Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Boniventure Masambu, amesema sampuli zote zilizochukuliwa kwa nyakati tofauti na kufanyiwa uchunguzi zimeonyesha kuwapo kwa kemili na hivyo kutoa ushauri.

    Naye Kaimu Meneja wa Acacia, Reuben Ngusaro, ameahidi kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa ilikuweza kukabiliana na athari zote za kimazingira zinazotoka na tope sumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako