• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mueller asema, Trump hajafutiwa lawama za kuzuia sheria katika uchunguzi wa Russia kuingilia uchaguzi wa Marekani

    (GMT+08:00) 2019-07-25 09:13:26

    Mshauri maalum wa zamani wa Marekani Robert Mueller amesema, ripoti yake ya uchunguzi juu ya Russia haikumtoa lawamani rais wa sasa wa Marekani Donald Trump kwa kuzuia utekelezaji wa sheria.

    Bw. Mueller amesema hayo mbele ya kamati ya sheria ya bunge la Marekani kuhusu uchunguzi wake wa tuhuma za Russia kuingilia uchaguzi wa rais wa Marekani wa mwaka 2016, na kama rais Trump alizuia sheria kutekelezwa. Amesema rais huyo hakutolewa lawamani kutokana na vitendo anavyodaiwa kuvifanya, na kwamba hakuwa tayari kusema kama rais Trump alifanya uhalifu.

    Mueller amesema Wizara ya Sheria haina mamlaka ya kumfungulia kesi rais aliyeko madarakani, lakini alisema huenda Trump anaweza kukabiliwa na vikwazo vya sheria atakapomaliza muda wake wa urais.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako